" MUHIMU KWA MASHUJAA WOTE WANAJUMUIYA WA SMAUJATA NCHINI

MUHIMU KWA MASHUJAA WOTE WANAJUMUIYA WA SMAUJATA NCHINI

Niwaombe mashujaa kote nchini kwasasa tuwe watulivu na wasikivu kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama katika maelekezo yake ambayo vinaendelea kuyatoa, ni imani yangu kwakuwa serikali inao watalaam wa mambo haya itakuja na tathmini pamoja na njia sahihi za suluhu  kuyanusuru yasijirudie ama yasiendelee na endapo tutakuwa sehemu ya timu ya kitaifa  itakayoendesha maridhiano basi huko SMAUJATA kama sehemu ya jamii tutapata nafasi nzuri ya kushauri mojakwamoja. 

Hivyo rai yangu ni kuwa, tuepuke  mijadala hii pia wakati kama huu ambao uchunguzi na hatua  vinaendelea kwakuwa mijadala hiyo inaweza kuibua taharuki zaidi kuliko kujenga uelewa wa pamoja ambao ndio msingi wa matamanio ya kila mmoja kuona Taifa letu likirejea katika hali ya utulivu na utengamano wa kisiasa, Kijamii na Kiuchumi.

>>>Shujaa Sospeter Mosewe Bulugu,

Mwenyekiti Taifa SMAUJATA

Mungu Ibariki Tanzania,

Mungu Ibariki Afrika.

HEKIMA NA UMOJA, USHINDI NA USHUJAA SMAUJATA 🇹🇿


Post a Comment

Previous Post Next Post