📌 *Majiko 1,583 kuuzwa na kusambazwa kwa bei ya ruzuku* .
📌 *Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya Tsh 11,200* .
📍 *HANANG*
Mkuu wa wilaya ya Hanang Mheshimiwa Almishi Hazali ametoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Hanang kujitokezo kwa wingi kununua majiko banifu ambayo yameanzwa kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku.
Wito huo umetolewa leo tarehe 20 Novemba, 2025 na Mheshimiwa Hazali alipofika katika Tarafa ya Katesh Kata ya Nangwa kijiji cha Nangwa kukagua na kufatilia utekelezaji wa mradi ambapo jumla majiko 1,583 yatasambzwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku wilaya nzima.
“Mradi huu unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ni mwendelezo wa juhudi za serikali katika kutunza mazingira na kuboresha afya za wananchi kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha ya umuhimu wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia”
Alisema Mhe. Hazali.
Akizungumza wakati wa uuzaji wa majiko hayo, msimamizi wa mradi kutoka REA, Ndugu Abdulrazack Mkomi amesema,
Serikali imeweke ruzuku ya asilimia 80 katika kila jiko ili kumpunguzia mwananchi hususani wa maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji gharama ya kununua jiko na hivyo badala ya mwananchi kununua jiko kwa Tsh 56,000 atanunua kwa Tsh 11,200 pekee.
Aidha, Mradi huu unakuja kubadilisha mtazamo wa wananchi katika matumizi ya nishati ya kuni na mkaa kutoka kutumia kuni na mkaa mwingi mpaka kutumia kuni na mkaa kidogo wakati wa kupika.
Majiko haya yametengenezwa kwa nyenzo ambazo zinasaidia jiko kuhifadhi joto kwa mda mrefu hivyo kupunguza matumizi makubwa ya mkaa na kuni
Aidha majiko haya hayatoi moshi na hivyo kupunguza uzalishaji wa sumu itokanayo na kuni na mkaa ambayo husababisha magonjwa yanayochangiwa na uchafuzi wa hewa ndani ya nyumba.
Mwisho.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
✉️ info@eastafricanspirits.com

Post a Comment