Na Mapuli Kitina Misalaba
Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga limeadhimisha miaka 95 tangu
kuanzishwa kwake, huku likijivunia mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa katika
kuboresha huduma za umeme, kuongeza idadi ya wateja na kutekeleza miradi ya
kimkakati inayolenga kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini.
Akizungumza
katika maadhimisho hayo, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Hadija
Mbaruki, amesema shirika hilo limeendelea kufanya vizuri katika utoaji wa
huduma kwa wateja na utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku, huku
likisimamia miradi mikubwa inayolenga kuboresha upatikanaji wa umeme katika
Mkoa wa Shinyanga na mikoa jirani.
Amesema Mkoa
wa Shinyanga hupokea umeme kutoka katika gridi ya taifa unaotoka Dodoma kupitia
Singida, ambao husambazwa kwenda maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa na mikoa ya
Magharibi, huku kukiwa na miradi mingine ya kimkakati ikiwemo mradi wa umeme wa
jua uliopo Kishapu.
Mhandisi
Mbaruki amesema ongezeko la mahitaji ya umeme limeendelea kuonekana kupitia
idadi ya wateja wanaounganishwa na huduma hiyo kila mwaka, akibainisha kuwa
hadi Juni 2025 TANESCO Shinyanga ilikuwa na wateja 111,807, Juni 2026 wateja
waliongezeka na kufikia 127,000, na kwa sasa idadi hiyo imefikia takribani
136,000.
Ameeleza
kuwa ongezeko hilo ni ishara ya kukua kwa mahitaji ya umeme na juhudi za
shirika katika kuwafikia wananchi wengi zaidi, huku akiwashukuru viongozi wa
Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira yanayowezesha maendeleo ya sekta ya
nishati.
Aidha,
amesema ushirikiano wa TANESCO na Benki ya CRDB katika mpango wa ufadhili wa
uunganishaji umeme kwa wananchi ni hatua muhimu inayolenga kuondoa vikwazo vya
gharama na kuwawezesha wananchi wengi zaidi kupata huduma hiyo.
Kupitia
mpango huo, uliozinduliwa Oktoba 2, 2026, kaya zinazostahili katika maeneo ya
vijijini zinatarajiwa kunufaika na ruzuku ya Shilingi 27,000 kwa ajili ya
gharama za kuunganishiwa umeme, huku wananchi wa mijini na maeneo mengine
wakipata fursa ya mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kuunganishiwa huduma
hiyo
Mhandisi
Mbaruki amesema ushirikiano huo unaongeza hamasa katika utendaji wa shirika na
kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya
umeme kwa urahisi zaidi.
Ameongeza
kuwa TANESCO imeendelea kuboresha mifumo ya huduma kwa wateja, ikiwemo
mabadiliko kutoka mifumo ya analogia kwenda mifumo ya kidijitali, ambayo
imeongeza ufanisi na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa haraka.
Katika hatua
nyingine, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia
Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuunga mkono maendeleo ya sekta ya nishati,
ikiwemo hamasa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia inayolenga kulinda afya
za wananchi na mazingira.
Meneja huyo
ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na TANESCO katika kulinda
miundombinu ya umeme, kutoa taarifa za changamoto zinazojitokeza na kuepuka
vitendo vya uharibifu vinavyoweza kuathiri huduma.
Kwa upande
wake, Afisa Mahusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Emma
Nyaki, amesema shirika hilo linaendelea kuimarisha mahusiano na wananchi
kupitia huduma mbalimbali na shughuli za kijamii zinazolenga kuwafikia watu
wenye mahitaji maalumu.
Katika
maadhimisho hayo, TANESCO Mkoa wa Shinyanga imetoa jumla ya Shilingi 580,000
kwa ajili ya kuwasaidia wazazi wa watoto wachanga 27 ambao wamezaliwa leo, na kwamba kila mzazi atapatiwa tokeni ya
umeme yenye thamani ya Shilingi 20,000 kwa ajili ya kumwangazia mtoto wake.
Aidha,
watoto wamepatiwa huduma za chakula na vinywaji katika tukio hilo, hatua
iliyoonesha namna shirika hilo linavyoendelea kushiriki katika shughuli za
kijamii na kugusa maisha ya wananchi.
Muuguzi
Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kambarage, Paulina Kitambi, ameeleza umuhimu wa
ushirikiano huo katika kuwasaidia watoto na wazazi, huku akitoa shukrani kwa
TANESCO kwa mchango wake.
Baadhi ya
wafanyakazi wa muda mrefu wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga wameeleza namna huduma
za umeme zilivyokuwa hapo awali na hali ilivyo sasa, wakibainisha mabadiliko
makubwa yaliyotokana na maendeleo ya teknolojia, ambayo yameongeza ufanisi wa
kazi na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja.
TANESCO Mkoa wa Shinyanga imeahidi kuendelea kuboresha huduma, kutatua changamoto zinazojitokeza na kuimarisha miundombinu ya umeme, huku wananchi wakihimizwa kuwa wavumilivu na kushirikiana na shirika hilo wakati jitihada za kutafuta ufumbuzi wa changamoto zikiendelea.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Hadija Mbaruki, akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 95 ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ambapo ameeleza mafanikio yaliyofikiwa na hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa kuboresha huduma za umeme.

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Hadija Mbaruki, akiwalisha keki baadhi ya wafanyakazi wakati wa maadhimisho ya miaka 95 ya TANESCO, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea safari ya shirika hilo na mafanikio yaliyofikiwa.

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Hadija Mbaruki, akiwa pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo wakigonganisha glasi za shampeni wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 95 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ikiwa ni ishara ya kusherehekea mafanikio na safari ya shirika hilo.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Hadija Mbaruki, akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 95 ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ambapo ameeleza mafanikio yaliyofikiwa na hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa kuboresha huduma za umeme.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Hadija Mbaruki, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo wakati wa maadhimisho ya miaka 95 tangu kuanzishwa kwa TANESCO.

Watumishi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga wakiandaa mtoli kwa ajili ya watoto wachanga katika Kituo cha Afya Kambarage, ikiwa ni sehemu ya shughuli za kijamii zilizoambatana na maadhimisho ya miaka 95 ya shirika hilo.
Afisa Mahusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Emma Nyaki, akikabidhi msaada kwa niaba ya shirika hilo kwa ajili ya kuwasaidia wazazi wa watoto wachanga katika Kituo cha Afya Kambarage, wakati wa maadhimisho ya miaka 95 ya TANESCO.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 08
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment