" KATIBU WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM MPANDA JIMOTOLI MADUKA ATEMBELEA CHUO CHA KISDES, WANAFUNZI 40 WAANDIKISHWA

KATIBU WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM MPANDA JIMOTOLI MADUKA ATEMBELEA CHUO CHA KISDES, WANAFUNZI 40 WAANDIKISHWA

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, ametembelea Chuo cha Afya cha Katavi Institute of Science and Development Studies (KISDES), kilichopo Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, kwa ajili ya kutoa elimu na kuandikisha wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ziara hiyo iliyofanyika Novemba 19, 2026, imelenga pia kukutana na uongozi, walimu na wanafunzi wa chuo hicho na kutoa elimu kuhusu masuala ya elimu, malezi, mazingira, afya na utamaduni, pamoja na kueleza utaratibu wa uanachama wa CCM na jumuiya zake.

Katika mazungumzo yake na wanafunzi, Maduka alieleza kuhusu nafasi ya Jumuiya ya Wazazi CCM na Umoja wa Wazazi wa Tanzania, akiwafahamisha wanafunzi utaratibu wa kujiunga na jumuiya hiyo, kupata kadi za uanachama na umuhimu wa kutimiza wajibu wa kulipa ada kwa mujibu wa taratibu za jumuiya.

Kupitia zoezi hilo, jumla ya wanafunzi 40 waliandikishwa kuwa wanachama wapya. Wanafunzi hao walipata fursa ya kufahamu taratibu za uanachama na kueleza umuhimu wa kuendelea kupata elimu kuhusu CCM na jumuiya zake katika maeneo ya shule na vyuo.

Akizungumza kuhusu zoezi hilo, Maduka alisisitiza umuhimu wa viongozi wa jumuiya kuendelea kuwafikia wananchi ana kwa ana katika maeneo mbalimbali, ikiwemo vyuo, shule na makazi, ili kutoa elimu ya uanachama na kusaidia wanaotaka kujiunga kufuata taratibu zinazotakiwa.

Aidha, aliwahimiza makatibu wa Jumuiya ya Wazazi katika ngazi za kata kuweka kipaumbele katika shughuli za uandikishaji na uhamasishaji wa wanachama, kwa kushirikiana na viongozi pamoja na maafisa TEHAMA wa CCM Wilaya ya Mpanda.

Kwa upande mwingine, uongozi wa chuo hicho ulimpokea Katibu huyo, huku ziara hiyo ikitoa nafasi ya kuimarisha mawasiliano na mahusiano kati ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda na taasisi hiyo ya elimu.

Zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda katika kuendeleza elimu ya uanachama na usajili wa wanachama wapya katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Chuo cha Afya cha Katavi Institute of Science and Development Studies (KISDES), kilichopo Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Novemba 19, 2026.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Afya cha Katavi Institute of Science and Development Studies (KISDES), Ndg. Jenester Ntambi, mara baada ya kuwasili ofisini kwake chuoni hapo, kilichopo Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi.


Mkuu wa Chuo cha Afya cha Katavi Institute of Science and Development Studies (KISDES), kilichopo Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jenester Ntambi, akifurahia kumpokea Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, aliyetembelea chuo hicho kwa ajili ya kusalimia walimu na wanafunzi pamoja na kutoa elimu kuhusu elimu, malezi, mazingira, afya, utamaduni na uanachama wa Chama Cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akiwa katika kikao cha pamoja na Mkuu wa Chuo cha Afya cha Katavi Institute of Science and Development Studies (KISDES), Ndg. Jenester Ntambi, pamoja na viongozi wa wanafunzi wa chuo hicho, kilichopo Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa wanafunzi wa Chuo cha Afya cha Katavi Institute of Science and Development Studies (KISDES), ofisini kwake chuoni hapo, Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akisalimiana na kujitambulisha kwa uongozi wa Chuo cha Afya cha Katavi Institute of Science and Development Studies (KISDES) pamoja na viongozi wa Serikali ya Wanafunzi, mara baada ya kuwasili chuoni hapo, Novemba 19, 2026.




Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, tarehe 19 Novemba 2026 akiwakabidhi Kadi za Umoja wa Wazazi wa Tanzania wanafunzi wa Chuo cha Afya cha Katavi Institute of Science and Development Studies (KISDES), kilichopo Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, baada ya kujiandikisha kuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda.


Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Chuo cha Afya cha Katavi Institute of Science and Development Studies (KISDES), Ndg. Jenester Ntambi, pamoja na wanafunzi wa chuo hicho, wakati wa ziara yake chuoni hapo tarehe 19 Novemba 2026.

Mwl. Isack Kyando wa Chuo cha Afya cha Katavi Institute of Science and Development Studies (KISDES), akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo hicho waliojiandikisha kuwa wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi.


Wanafunzi wa Chuo cha Afya cha Katavi Institute of Science and Development Studies (KISDES) wakiwa katika shughuli za kutoa hamasa na kuwakaribisha wazazi, walezi na wanafunzi kutoka Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi na maeneo mengine kujiunga na chuo hicho kinachotoa elimu ya afya. Chuo hicho kipo Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, kikilenga kutoa fursa ya kupata elimu ya juu.

Wanafunzi wa Chuo cha Afya cha Katavi Institute of Science and Development Studies (KISDES) wakiwa katika mafunzo kwa vitendo (practical) ya masomo darasani, yanayowawezesha kupata ujuzi na uzoefu katika fani ya afya. Chuo kinawakaribisha wazazi, walezi na wanafunzi kujiunga ili kushiriki katika kukuza maendeleo ya elimu, hususan katika sekta ya afya.

Wanafunzi wa Chuo cha Afya cha Katavi Institute of Science and Development Studies (KISDES) wakiwa katika shughuli za masomo darasani, wakijifunza kwa bidii na kujituma ili kufanikisha malengo yao ya kielimu. Chuo kinawakaribisha wanafunzi wapya kujiunga na kusoma kwa pamoja, kwa lengo la kukuza elimu na kuleta maendeleo katika sekta ya afya.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akiagana na Mkuu wa Chuo cha Afya cha Katavi Institute of Science and Development Studies (KISDES), Ndg. Jenester Ntambi, mara baada ya kumaliza ziara yake chuoni hapo tarehe 19 Novemba 2026.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 08

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post