Na Mapuli
Kitina Misalaba
BALOZI wa
Sweden nchini Tanzania, Ingrid Teresia Johansson, akiambatana na mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), Ms. Lorence
Ansermet, wametembelea kiwanda cha Jambo Group mkoani Shinyanga kwa lengo la
kujadili fursa za ushirikiano katika kuwawezesha wafugaji wadogo na kuboresha
mifumo ya ukusanyaji wa maziwa.
Ziara hiyo
imefanyika leo Jumatatu, Novemba 16, 2026, ambapo viongozi hao wamejadiliana na
uongozi wa kampuni hiyo kuhusu namna ya kuimarisha upatikanaji wa maziwa kutoka
kwa wafugaji, kuboresha vituo vya kukusanyia maziwa pamoja na kuongeza
uzalishaji viwandani.
Akizungumza
katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, amesema
Serikali inathamini juhudi za kuimarisha mahusiano ya Tanzania na mataifa
mengine, akieleza kuwa ushirikiano huo unaweza kufungua fursa zaidi za
maendeleo ya viwanda na sekta ya ufugaji.
Mtatiro
amesema kiwanda cha Jambo Group kina mchango katika kuongeza thamani ya mazao
ya mifugo, hususan maziwa, ambapo katika kipindi cha takribani mwaka mmoja na
nusu uliopita kimepanua wigo wa uzalishaji kwa kuanza kuzalisha maziwa na
bidhaa nyingine zinazotokana na maziwa.
Amesema kwa
sasa kiwanda hicho kinaendelea na juhudi za kuhakikisha kinapata takribani
asilimia 80 ya mahitaji yake ya maziwa kutoka kwa wafugaji wa ndani, huku
akieleza kuwa ushirikiano na Sweden pamoja na UNIDO unaweza kusaidia kuimarisha
mnyororo wa thamani katika sekta hiyo.
Kwa upande
wake, Afisa wa Jambo Group, Mussa Riobo, amesema ziara hiyo imelenga kujadili
namna ya kuwawezesha wafugaji wadogo kuboresha ufugaji wao pamoja na kuimarisha
vituo vya kukusanyia maziwa vinavyojulikana kama TENKAS ili viendane na mifumo
ya kisasa.
Ribo amesema
kiwanda kinakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maziwa ya kutosha, hali
inayosababisha uzalishaji kusimama kwa nyakati fulani kutokana na uhaba wa
malighafi hiyo.
Amesema kwa
sasa kiwanda kinazalisha takribani lita 30,000 za maziwa kwa siku, wakati
mashine zake zina uwezo wa kuzalisha hadi lita 100,000 kwa siku, hivyo kuna
umuhimu wa kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa maziwa ili kuhakikisha kiwanda
kinakuwa na malighafi ya kutosha kwa ajili ya uzalishaji endelevu.
Amesema
maboresho ya vituo vya ukusanyaji wa maziwa yatasaidia kuongeza kiwango cha
maziwa kinachokusanywa kutoka kwa wafugaji na kuhakikisha kiwanda kinaendelea
na uzalishaji bila kusimama kutokana na upungufu wa malighafi.
Aidha Ms.
Lorence Ansermet ni mwakilishi wa UNIDO anayesimamia shughuli za shirika hilo
katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi, Mauritius, Seychelles na Umoja wa
Visiwa vya Comoro.
Wawakilishi wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, UNIDO, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga pamoja na viongozi wa Jambo Group wakielekea kiwandani kuanza ziara ya kutembelea na kujadili fursa za ushirikiano katika sekta ya ufugaji na uzalishaji wa maziwa.
Wawakilishi wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania, UNIDO, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga pamoja na viongozi wa Jambo Group wakielekea kiwandani kuanza ziara ya kutembelea na kujadili fursa za ushirikiano katika sekta ya ufugaji na uzalishaji wa maziwa.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania, wawakilishi wa UNIDO na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakipokea maelezo kutoka kwa viongozi wa Jambo Group kuhusu shughuli za uzalishaji, uwezo wa kiwanda na mifumo ya ukusanyaji wa maziwa kutoka kwa wafugaji.
Viongozi wa Jambo Group, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, wawakilishi wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania pamoja na Shirika la UNIDO wakitembelea kiwanda cha Jambo Group mkoani Shinyanga kujadili fursa za ushirikiano katika kuimarisha sekta ya ufugaji na uzalishaji wa maziwa.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania, wawakilishi wa UNIDO na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakipokea maelezo kutoka kwa viongozi wa Jambo Group kuhusu shughuli za uzalishaji, uwezo wa kiwanda na mifumo ya ukusanyaji wa maziwa kutoka kwa wafugaji.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akizungumza kuhusu umuhimu wa ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden katika kufungua fursa za maendeleo ya viwanda na kuwawezesha wafugaji.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Ingrid Teresia Johansson, akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea kiwanda cha Jambo Group mkoani Shinyanga, ambapo ameeleza fursa za ushirikiano katika kukuza sekta ya ufugaji na uzalishaji wa maziwa.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), Ms. Lorence Ansermet, akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea kiwanda cha Jambo Group mkoani Shinyanga.
Afisa wa Jambo Group, Mussa Riobo, akielezea shughuli za uzalishaji kiwandani pamoja na changamoto ya upatikanaji wa maziwa ya kutosha kutoka kwa wafugaji.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254










Post a Comment