" SIMBA SC YAKUBALI KIPIGO NYUMBANI DHIDI YA PETRO ATLETICO DE LUANDA, LIGI YA MABINGWA AFRIKA

SIMBA SC YAKUBALI KIPIGO NYUMBANI DHIDI YA PETRO ATLETICO DE LUANDA, LIGI YA MABINGWA AFRIKA






Klabu ya Simba SC imepoteza kwa bao 1–0 dhidi ya Petro Atletico de Luanda katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa leo, Novemba 23, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa dakika ya 78 na kiungo Benardo Oliveira Dias, maarufu kama “Benny”, akiipatia Petro Atletico ushindi muhimu ugenini.

Simba ilijitahidi kusaka bao la kusawazisha katika dakika za mwisho, lakini ukuta wa Petro ulibaki imara huku kipa wao akifanya kazi ya ziada kuzuia jaribio la mwisho la Moses Phiri.

Kwa matokeo haya, Wekundu wa Msimbazi wanalazimika kusaka ushindi katika michezo yao ijayo ili kuongeza matumaini ya kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment

Previous Post Next Post