Na Meleka Kulwa -Dodoma
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 14,2025 Jijini Dodoma, mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa vurugu zilizoibuka baada ya uchaguzi zilisababisha uharibifu wa mali, kupoteza maisha na kuhatarisha usalama wa nchi.
Amesema kuwa baadhi ya vijana waliojumuika katika vurugu hizo walifuata mkumbo bila kujua uzito wa matendo waliyokuwa wakiyafanya.
Aidha, amebainisha kuwa kama mlezi wa taifa, amevielekeza vyombo vya sheria—hasa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)—kuangalia kwa makini viwango vya makosa yaliyofanywa na vijana hao, na kwamba wale walionekana kuingia katika vurugu kwa ushabiki bila dhamira ya kufanya uhalifu waachiwe waende kwa wazazi wao.
Aidha,Rais Samia amesema kuwa nchi imejengwa juu ya misingi ya amani na utulivu wa kisiasa, na kwamba vijana wasikubali kushawishiwa kuharibu nchi yao wenyewe.
Aidha, amebainisha kuwa hatua ya kutoa msamaha kwa vijana hao imetokana na ukweli kwamba wengi wao hawakujua walichokuwa wakikitenda, akirejea pia maneno ya maandiko matakatifu yanayosema, “Baba uwasamehe kwa kuwa hawajui watendalo.”
Aidha,, amesema kuwa kama wazazi wao wangefanya vurugu kama zile zilizoshuhudiwa majuzi wakati wa ujana wao, leo wasingekuwa na fursa ya kuishi maisha ya amani, kuoa, kupata watoto na kuwalea kama ilivyo sasa.
Amebainisha kuwa vijana ndio walinzi na wajenzi wa taifa, hivyo wasiwe sehemu ya kulibomoa bali kulijenga kwa kuzingatia busara, maelewano na uzalendo.
Post a Comment