" WANANCHI WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUPATA HUDUMA BURE ZA MAGONJWA YASIYOYAKUAMBUKIZA SHINYANGA

WANANCHI WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUPATA HUDUMA BURE ZA MAGONJWA YASIYOYAKUAMBUKIZA SHINYANGA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Luzila John, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi katika kambi ya afya inayoendelea katika viwanja vya Zimamoto, Nguzonane, mjini Shinyanga, ili kupata elimu na huduma za uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza bila malipo.

Akizungumza leo na vyombo vya habari, Dkt. Luzila amesema Tanzania huadhimisha Siku ya Magonjwa Yasiyoambukiza Duniani kila wiki ya pili ya mwezi wa Novemba, ambapo mwaka huu maadhimisho hayo yanafanyika kuanzia Novemba 10 hadi 15, 2025, yakiwa na kauli mbiu “CHUKUA HATUA DHIBITI MAGONJWA YASIYOYAKUAMBUKIZA.”

Amesema Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga imeshiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo kwa kutoa elimu na huduma za uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya figo, kansa, sikoseli na magonjwa sugu ya mapafu.

“Natoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kupima afya zao, kujifunza namna ya kujikinga na kuishi salama endapo watabainika kuwa na magonjwa haya. Magonjwa yasiyoambukiza husababishwa zaidi na mtindo wa maisha, hivyo elimu ni silaha muhimu ya kinga,” amesema Dkt. Luzila.

Amefafanua kuwa kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa Septemba 25, 2025, takribani vifo milioni 43 duniani vimetokana na magonjwa yasiyoambukiza, ambapo magonjwa ya moyo yanayoambatana na shinikizo la damu yanaongoza kwa kusababisha vifo vingi zaidi.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kambi hiyo wameishukuru Serikali kupitia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kwa kuratibu huduma hizo bure, huku wakipongeza uwepo wa wataalamu wa lishe na madaktari bingwa wanaotoa huduma kwa ukaribu na uelewa.

Kambi hiyo ya afya imeanza leo Jumatatu, Novemba 11, 2025 na inatarajiwa kukamilika Jumamosi wiki hii, ambapo zaidi ya watu miani tano (500) wanatarajiwa kupata huduma za uchunguzi na elimu ya afya.


 

1 Comments

  1. Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

    Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

    Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ndiyo tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

    Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

    Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

    Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159

    ReplyDelete

Post a Comment

Previous Post Next Post