" Basata Watoa Sababu za Kuhairisha Tuzo za Music za TMA

Basata Watoa Sababu za Kuhairisha Tuzo za Music za TMA

 

Baraza la Sanaa la Taifa ‘Basata’ limetangaza kuahirisha halfa ya ugawaji tuzo za TMA ilizokuwa ikitarajia kufanyika  Desemba 13,2025.

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa leo Desemba 13,2025 kwenye ukurasa wao wa Instagram imeomba radhi kwa kutokuwa na hafla hiyo

“Tunawataarifu kuwa hafla ya TMA iliyokuwa imepangwa kufanyika tarehe 13/12/2025 imeahirishwa mpaka pale tarehe nyingine itakapotangazwa. Tunaomba Radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza”imeeleza taarifa hiyo

Hata hivyo akizungumza na Mwananchi Edward Buganga ambaye ni Mkurugenzi wa Ukuzaji na Maendeleo ya Sanaa Basata amesema bado kuna mambo hayajakaa sawa

“Tumeahirisha tutatangaza, mazingira yenyewe si unayaona kipindi hiki. Bado maandalizi yetu hayajakaa vizuri yanahitaji ufadhili na mambo mengi kwahiyo bado tupo kwenye maandalizi tunaweka mambo vizuri,”amesema Buganga

Ikumbukwe Tuzo za muziki Tanzania (TMA) zilianzishwa mwaka 1999 na Baraza la Sanaa la Taifa BASATA ili kutambua vipaji na ubunifu katika kiwanda cha muziki nchini ambapo zilidumu kwa miaka 16, kuanzia 1999 hadi mwaka 2015.

Tuzo hizo hapo awali zilitambulika kama Kilimanjaro Music Awards ‘Kili Music Awards’ zilirudi tena mwaka 2022 na kutambulika kama Tanzania

Music Awards TMA baada ya kutofanyika kwa miaka saba mfululizo tangu mwaka 2015 hadi 2022.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post