Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaMsani wa kizazi kipya na Kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi ,anayetambulika kwa jina maarifu la "Bobi Wine", chini Humo na hata nje ya Uganda ametoa wito kwa Rais Yoweri Museveni na vyombo vya dola kuepuka matumizi ya nguvu Kali dhidi ya raia wakati nchi ikielekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Januari 2026.Kina huyo ameyasena hayo Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), amesema kuwa harakati anazoongoza hazilengi kuchochea vurugu bali zinatetea haki ya wananchi kufanya maandamano ya amani, haki inayotambuliwa na Katiba ya Uganda.Aidha amesema wito wake unawalenga raia wa kawaida wanaotafuta haki, na si makundi ya wahuni wanaohusishwa na vitendo vya uvunjifu wa amani.Kiongozi huyo wa chama cha National Unity Platform (NUP) amesema maandamano hayatakuwa muhimu endapo serikali itahakikisha uchaguzi huru, wa haki na wa uwazi.Sambamba na wito wake kwa Rais wa Uganda ameituhumu serikali ya Rais Museveni kwa kuzuia shughuli za kampeni za upinzani, kufungia baadhi ya vituo vya redio na kuwakamata au kuwatisha wafanyakazi wa kampeni za vyama pinzani.
Msani wa kizazi kipya na Kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi ,anayetambulika kwa jina maarifu la "Bobi Wine" 🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment