Katibu wa Jumuiya ya wazazi wa CCM Wilaya ya Mpanda Jimotoli Jilala Maduka akizungumza. Katibu wa Jumuiya ya wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi Jimotoli Jilala Maduka amewashukuru wananchi wa Kijiji cha Milala kwa kuridhia kwa pamoja kupitia upya mipaka ya shule ya sekondari Milala ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuifufua shule hiyo iliyochini ya jumuiya ya wazazi.Katibu wa Jumuiya ya wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi Jimotoli Jilala Maduka amewashukuru wananchi wa Kijiji cha Milala kwa kuridhia kwa pamoja kupitia upya mipaka ya shule ya sekondari Milala ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuifufua shule hiyo iliyochini ya jumuiya ya wazazi.Jilala ametoa pongezi hizo kwenye mkutano wa kijiji hicho kilichofanyika kijijini hapo ambapo wananchi kwa pamoja wameruhusu kupitia upya mipaka ya eneo hilo la shule ili kuruhusu mchakato wa kuanza kwa shule hiyo kufanya kazi kwa maslahi mapana ya kijiji katika kukuza elimu kupitia shule hiyo.
‘’Katika upimaji huo wote tukawe mashuhuda shule ya sekondari Milala ianze kufanya kazi na kipindi tutakapo peleka mhutasari huu wa wananchi imekaa vizuri itakuwa ni jambo la kushukuru Mungu tukileta mwekezaji hapa shule itaanza kufanya kazi watoto wenu watasoma hapa’’ amesema Jilala.
Aidha amesema Jumuiya ya wazazi pamoja na serikali kwa pamoja wamejipanga kuhakikisha maendeleo yanakuja milala kupitia sekta ya Elimu na jumuiya ya wazazi moja ya jukumu lake ni kusimamamia elimu
Ameeleza kuwa moja mipango ya serikali ya Rais Dkt Samia suluhu Hassan kuimarisha miundombinu ya elimu kwa kusogeza huduma hizo karibu na wananchi kwa maendeleo endelevu katika jamii na taifa kwa ujumla.
Veronica Lemi Mwenyekiti wa kijiji cha Milala amesema mpango huo wa jumuiya ya wazazi ya kupitia eneo hilo upya la shule ya sekondari Milala unatija kubwa kwa maendeleo ya kijiji kwakuwa wanananchi watawapeleka watoto wao hapo kwaajili ya kupata elimu.
Lemi amekiomba chama cha Mapinduzi hususani Jumuiya ya wazazi kuharakisha mpango huo kwakuwa wananchi kwa pamoja wameridhia kufanya mapitio ya mipaka hiyo ili kuruhusu hatua za mwekezaji kuanza kazi kwenye shule hiyo.
Nao baadhi ya wananachi wa Kijiji cha Milala wameishukuru Jumuiya ya wazazi kwa kuja na mpango huo mahususi kwani wanafunzi wa kijiji hicho wamekuwa wakikatiza masomo ya sekondari kwa kukosa sekondari iliyopo karibu.
‘’Tunashukuru sana kwakweli sisi wananachi tunafurahi kuona mchakato huu umeanza maana ukifika eneo la shule limegeuka poli ila kwa mpango huu nauona mwanga mpya kwenye shule hii anasema Khamis Juma Mkazi wa Milala .
Kuanza kwa hatua hizo za kupitia upya mipaka ya eneo hilo la sekondari ya milala ni ishara njema kwa kuanza kwa hatua mpya za kuifufua shule hiyo ambayo inatajwa kuwa kongwe katika Wilaya ya Mpanda eneo hilo la shule ya sekondari milala linaukubwa wa hekali 135.91
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Milala pamoja na viongozi wa Kijiji hicho wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Mpanda Jimotoli Jilala baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Katibu wa Jumuiya ya wazazi wa CCM Wilaya ya Mpanda Jimotoli Jilala Maduka, akiwa ofisini.

Picha ya pamoja.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment