Na Lydia Lugakila, Misalaba Media MbeyaLeo ikiwa ni Desemba 9, siku ya maadhimisho ya Uhuru, wakazi wengi wamesalia majumbani wakipumzika huku wengine wakiendelea na shughuli zao kama kawaida.Hali ya usalama katika Jiji la Mbeya imeendelea kuwa shwari, licha ya taarifa kwamba baadhi ya watu walipanga kufanyika kwa maandamano yasiyokoma.Katikati ya Jiji la Mbeya—hasa katika maeneo ya Posta—hali ya utulivu iko shwari asilimia 100. Mitaa ya Posta, maarufu kwa kuwa kitovu cha ofisi za serikali pamoja na wafanyabiashara wakubwa, imeonekana kuwa tulivu na shughuli zikiendelea kwa utaratibu.Aidha, Barabara na mitaa inayoelekea Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine inaendelea kuwa salama, ikiwemo Barabara ya Karume inayoingia City Centre, ambapo hali ya usalama imeripotiwa kuwa thabiti.Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment