Na Lydia Lugakila, Misalaba Media
Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo LULU SACCOS LTD kutoka Mkoani Mbeya kimejipanga kufungua tawi mkoani Dar es Salaam ifikapo mwaka 2026 endapo kitafanikiwa kuondoa fungamano la ushirika linalowalenga wafanyabiashara na wajasiriamali waishio ndani ya Mkoa wa Mbeya.
Kauli hiyo imetolewa na Oberd Mtweve, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya LULU SACCOS iliyopo Soweto, Kata ya Ruanda jijini Mbeya, wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake waliotaka kujua mambo mbalimbali kuhusu chama hicho.
Mtweve amesema kuwa moja ya malengo waliyojiwekea kwa mwaka 2026 ni kuondoa fungamano la ushirika linalowataka wanachama kufanya kazi Mbeya pekee, ili kuruhusu kufungua tawi Dar es Salaam na kusogeza huduma karibu na wanachama.
Amesema tayari wana wanachama takribani 27 ambao wanaishi Mbeya na Dar es Salaam.
"Nadhani wale walioko Dar es Salaam tutawapa nafasi ya kuendelea kutafuta wanachama wengine ambao ni waadilifu tutakaoanza nao kufungua tawi hilo," alisema Mwenyekiti wa Bodi ya Lulu Saccos.
Aidha, amesema watatoa kipaumbele kwa kuanza na wanachama 100 kwa tawi la Dar es Salaam na kwamba tayari wamepokea maombi kutoka kwa watu wa mikoa mbalimbali walioonesha nia ya kujiunga na Lulu Saccos licha ya fungamano kuwa kikwazo.
Hata hivyo, amesema kuwa kwa sasa wana jumla ya wanachama 536 mkoani Mbeya, na ameahidi kuendelea kuwahudumia wanachama wote kwa uadilifu na uwajibikaji.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment