" MASAUNI ACHAGULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS BARAZA LA MAZINGIRA LA UMOJA WA MATAIFA

MASAUNI ACHAGULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS BARAZA LA MAZINGIRA LA UMOJA WA MATAIFA






……………

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA).

Hayo yamejiri katika mkutano wa saba wa Baraza hilo uliofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), jijini Nairobi, Kenya Desemba 12, 2025.

Uchaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 18 ya Kanuni za Utendaji za UNEP inayotaka Baraza kumchagua Rais, Makamu wa Rais pamoja na Mwandishi katika kikao cha mwisho cha mkutano wake.

Aidha, Mhandisi Masauni amependekezwa na Kundi la Nchi za Afrika, ambalo kwa kuzingatia kanuni za mzunguko na uwakilishi wa kijiografia, limepewa nafasi mbili za Makamu wa Rais katika Ofisi ya Baraza hilo.

Uchaguzi wake umeidhinishwa bila kupingwa, hatua inayodhihirisha imani na heshima kubwa ya jumuiya ya kimataifa kwa uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika masuala ya mazingira, mabadiliko ya tabianchi na maendeleo endelevu.

Kuchaguliwa kwa Waziri kushika wadhifa huo ni heshima kubwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na unaakisi dhamira, mchango na msimamo thabiti wa nchi katika kutekeleza sera, mikakati na ahadi za kikanda na kimataifa kuhusu ulinzi na uhifadhi wa mazingira.

Halikadhalika, katika uchaguzi huo Waziri wa Maji, Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi wa Jamaica Mhe.Matthew Samuda amechaguliwa kuwa Rais Baraza hilo baada ya kupendekezwa na Kundi la Nchi za Amerika ya Kusini na Karibiani.

Pia, Vilevile, Baraza limemchagua Balozi wa Masuala ya Mazingira na Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kimataifa katika Shirika la Mazingira la Uswisi Mhe. Felix Wertli kuwa Mwandishi wa Baraza hilo. Mhe. Wertli amependekezwa na Kundi la Nchi za Ulaya Magharibi na Nyinginezo.

Mkutano wa saba wa UNEA uhitimishwa rasmi Desemba 12, 2025 ambapo Ofisi mpya ya Baraza itachaguliwa kuhudumu katika kikao cha nane cha UNEA.

Mkutano uliwakutanisha wakuu wa nchi na serikali, mawaziri wanaoshughulikia mazingira, wataalam na wadau wa Mazingira na maendeleo endelevu kutoka nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa, Mashirika ya Umoja wa Mataifa na asasi za kiraia.

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Mhe. William Lukuvi aliyemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Viongozi wengine waliohudhuria nia pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja na wataalamu mbalimbali kutoka Ofisi hiyo.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post