Na Fabius Clavery -Misalaba Media, Kagera.Serikali ya Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na Baraza la Biashara la Mkoa huo imeweka mipango ya kuanzisha na kupanua fursa za ajira kwa vijana kupitia biashara, uwekezaji na matumizi ya teknolojia za kisasa ili kukuza uchumi wa mkoa.Akifungua kikao cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Kagera kilichofanyika Desemba 18, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatuma Mwassa amesema vijana ni rasilimali muhimu kwa maendeleo ya taifa, hivyo wanapaswa kuwezeshwa kiuchumi kupitia ajira zenye staha.Amesema vijana wanachangia takribani asilimia 34 ya idadi ya watu wa mkoa huo, akisisitiza umuhimu wa kubainisha fursa zilizopo na kuziwekea mikakati madhubuti ili kuondoa tatizo la nguvu kazi kubwa isiyo na ajira.“Vijana wakipata ajira, pato la mtu mmoja mmoja linaongezeka na uchumi wa mkoa unakua. Lengo letu ni kuondoa hali ya kuwa na nguvu kazi kubwa isiyo na ajira,” amesema.Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema Serikali itaendelea kutengeneza mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wawekezaji ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa na kuongeza pato la taifa.Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kagera na mjumbe wa Baraza la Biashara, Castro John, amesema mamlaka hiyo inaendelea kusikiliza na kutatua kero za wafanyabiashara, akibainisha kuwa changamoto kubwa kwa wafanyabiashara imekuwa ni ukosefu wa uelewa wa masuala ya kodi.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment