" Simba Wapunguza Bei ya Jezi Hadi 12000, Ahmedy Ally Afunguka

Simba Wapunguza Bei ya Jezi Hadi 12000, Ahmedy Ally Afunguka

 

“Tunachofanya Simba na JayRutty ni kwenda na kasi ya dunia. Tumeamua kufungua soko letu kwenye digital ili watu wapate jezi kwa urahisi. Tukienda na punguzo hili la jezi lakini pia tunarahisisha mtu kupata jezi yake.”

“Pamoja na kwamba tunatoa punguzo la msimu wa sikukuu lakini pia tunapambana na jezi fake. Kama Mwanasimba alikuwa ananunua jezi fake Tsh. 15,000 sasa jezi original ataipata kwa Tsh. 12,000. Uamuzi ni kwako Mwanasimba.”

“Bei hii ya punguzo inaanza leo Desemba 16, 2025 na itakwenda hadi Januari 30, 2026 hivyo tuna siku 45 za ofa hii. Na kuna watu wanakwenda nyumbani sikukuu, usikubali kwenda mikono mitupu, nunua jezi za Simba uende na zawadi.”

“Unaweza kupata jezi hii hata kwa kukopa. Mitandao yote ya simu wanakopesha wateja wao hivyo unaweza kukopa sasa na kupata jezi yako. Hii fursa hatupaswi kuichezea hata kidogo, huu ndio wakati wa kila Mwanasimba kununua jezi yake original.”

Post a Comment

Previous Post Next Post