Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Arusha Mjini, Paul Makonda, amewasihi Viongozi wa Jiji la Arusha, Wakuu wa Idara na Watumishi wa Umma kutimiza majukumu yao ipasavyo na kufanya kazi kwa bidii akisema ni aibu Mtumishi kusimamishwa na Viongozi wakuu na akaishia kuzomewa.
Akiongea na Wakuu wa Idara wa Jiji la Arusha, Makonda amesema “Sisi sio Watendaji, Mbunge wala Diwani sio Mtendaji wa kazi za kila siku, wewe (Mkuu wa Idara) ndio umeajiriwa kwa niaba yetu sasa pale wewe unayelipwa mshahara kwa niaba yetu sisi uwafanyie kazi Wananchi, kama kazi haziendi ndio mgogoro unapoanzia, ndio maana hata akija Kiongozi mkubwa kama alivyokuja Waziri Mkuu, unaweza kusimamishwa Wananchi wakaanza kukuzomea, infact ikifika hatua Mtumishi wa Umma unasimamishwa kwenye mkutano wa hadhara unaulizwa maswali Wananchi wanakuzomea yaani kiutaratibu unatakiwa kufukuzwa kazi hapohapo uwanjani”
“Maana yake hao wanatuma ujumbe kwamba hawafurahishwi na kazi yako na kama ingekuwa ni kupiga kura wewe hauna kura za Kiongozi aliyechaguliwa, mathalani kila Mkuu wa Idara hapa akisimama tukakuuliza wewe kwenye Idara yako unachangia asilimia ngapi ya ushindi wa Dkt. Samia?, mfano Mkuu wa Idara ya Ardhi tukikusimamisha kwa Wananchi wakaambiwa wapige kura una asilimia ngapi?



Post a Comment