Na:Belnardo Costantine, Misalaba MediaMamlaka za serikali nchini Ghana zimemkamata na kumfikisha kizuizini Nabii mwenye utata nchini humo aliyetambulika kwa Jina la Nabii Ebo Noah.Duru zinasema Nabii huyo amekamatwa Kwa kusabibisha taharuki baada Kueneza Taarifa za Uongo za kudai Dunia itangamia ifikapo tarehe 25/12/2025 mwaka huu kwa gharika ya mvua .Aidha baada kueneza taarifa hizo Nabii Ebo Noah alisema ameambiwa na Mungu na kumuagiza atengeze Safina kwa ajili ya kuwahifadhi watu baada ya Mungu kushusha gharika la mvua kubwa litakayoifuta Dunia tarehe 25 December 2025.Mamlaka nchini Ghana imesema kuwa taarifa hiyo feki kutoka Kwa Nabii huyo ya kudai Mungu atangamiza dunia kwa kutumia maji, imezua hofu kubwa na mvutano kwa wananchi nchini humo.Hatahivyo baadhi ya taarifa nchini Ghana zinaeleza kuwa kutokana na utabiri huo, watu kutoka maeneo mbalimbali wameanza kujiandaa kusafiri kwenda kuingia kwenye safina ambazo Nabii Ebo noah tayari amesha ziandaa na kuzijenga kwa ajili ya kuhifadhi watu siku hiyo.Sambamba na hilo mamlaka za kiusalama nchini Ghana zimekanusha vikali utabiri huo, zikieleza kuwa ni taarifa za uongo na zisizo na msingi🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment