" WATANZANIA WAKUMBUSHWA KUANGALIA MUSTAKABALI: AMANI NI JUKUMU LA KILA MMOJA

WATANZANIA WAKUMBUSHWA KUANGALIA MUSTAKABALI: AMANI NI JUKUMU LA KILA MMOJA

Kama Taifa, Watanzania wamekumbushwa kuacha kurudi nyuma na kuangalia Desemba 9, na badala yake, kuelekeza nguvu zote kwenye mustakabali wa maendeleo. Wananchi washikilie msimamo mmoja: amani ni jukumu la kila mmoja.

Mzazi Witness Lena wa Dar es Salaam anatoa wito wa uzalendo, akisema, “Wananchi wa Tanzania wameendelea kuwa mfano mzuri wa kuishi kwa amani... Licha ya uchaguzi mkuu, bado tunaweza kuishi kwa amani”. Anaongeza, “Ni jambo la kupongezwa kuona pamoja na matatizo madogo yanayotokea, bado watu wakiwa muda wa kuwa na umoja na ushirikiano”.

Ujumbe huu unaungwa mkono na Mzazi, Neema Simon, ambaye anakumbusha matukio yaliyopita: “Tunawashukuru wananchi hasa vijana kuendelea kulinda amani... kwa sababu bila amani, hakuna maisha”.

Ingawa Wananchi wanakiri uwepo wa makundi yenye nia mbaya. Mzazi Tito Nyingi wa Mbeya anasema, “Nikikumbuka kilichotokea baada ya uchaguzi [vurugu], tunaona kabisa siasa zinatishia amani yetu”. Wito wa pamoja ni kuacha “ugomvi” na “chuki” na kuacha kujihusisha na mambo yasiyokuwa ya lazima. Lengo ni moja: kuhakikisha familia na jamii zinaendelea kuishi kwa amani na utulivu.

Ni wakati wa Watanzania kukumbuka msingi wa nchi yao na kuacha kurudi nyuma. Baada ya nchi kushuhudia majaribio ya vurugu Oktoba 29 na Desemba 9 na utulivu kudumu .

Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene akizungumza kuhusu utulivu wa nchi, anasisitiza kuwa mustakabali wa Tanzania unategemea uwezo wa wananchi kuishi katika salama, utulivu, na kuheshimiana. Anakumbusha kwamba Wananchi wanapaswa  kurudi nyuma na kutafakari mustakabali wa nchi, kwani amani huanza na wewe.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post