MICHEZO.
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Jumamosi, Januari 17, 2026, imetangaza rasmi kufutwa kwa mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN).
Uamuzi huo umetolewa miezi mitano baada ya kumalizika kwa mashindano ya CHAN 2025, ambayo yaliandaliwa kwa pamoja na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, ambapo Morocco iliibuka bingwa.
Kwa mujibu wa CAF, mashindano hayo sasa yamefutwa kabisa, yakifikia tamati baada ya kuendeshwa kwa kipindi cha miaka 16, tangu yalipoanzishwa rasmi mwaka 2009.
Akizungumza kuhusu uamuzi huo, Rais wa CAF Patrice Motsepe amesema kuwa sababu kuu ya kufutwa kwa CHAN ni gharama kubwa za kifedha zinazotumika kuendesha michuano hiyo.
"Hakutakuwa na CHAN. Hakuna haja ya kuwa na CHAN. Ni Mashindano yanayopoteza fedha nyingi kwa kiwango kikubwa." amesema Motsepe.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment