Na Lydia Lugakila -Misalaba Media MbeyaMkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Uyole, Spika Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amegawa vifaa vya shule kwa wanafunzi wenye uhitaji katika Jimbo la Uyole.Kupitia mpango huo, Dkt. Tulia ametoa msaada wa sare za shule na daftari kwa wanafunzi elfu tatu (3,000) wenye uhitaji zaidi kutoka kata 13 za Jimbo la Uyole.Msaada huo ni muendelezo wa juhudi zake za kuwasaidia watoto wasio jiweza, hususan kipindi cha kufungua shule, ili kuhakikisha wanapata fursa sawa ya elimu.Akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa hivyo, Dkt. Tulia amewataka wazazi na walimu kuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kuhakikisha watoto wanahudhuria shule na kupata elimu bora.Amesisitiza kuwa ufaulu wa wanafunzi unategemea ushirikiano wa karibu kati ya walimu na wazazi katika kutimiza wajibu wao.Aidha, Dkt. Tulia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu, hususan katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu. Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imefanikiwa kujenga shule na madarasa pamoja na kuboresha miundombinu mingine ya elimu, jambo litakalosaidia kuinua kwa kasi sekta ya elimu na kuwahamasisha wanafunzi kufanya vizuri zaidi katika masomo yao.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment