Na Lydia Lugakila, Misalaba MediaMbeyaSpika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Jimbo la Uyole, Dkt. Tulia Ackson, ameungana na Wananchi wa kata za Isyesye na Ilemi Mkoani Mbeya kushiriki zoezi la usafi katika maeneo yaliyoathiriwa na janga la mafuriko.Hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa Januari 5, 2026, wakati alipowatembelea wananchi hao na kujionea athari za mafuriko yaliyosababisha uharibifu wa makazi na miundombinu pamoja na kusababisha usumbufu mkubwa kwa maisha ya kila siku ya wakazi wa maeneo hayo.Katika ziara hiyo, Dkt. Tulia aliwasilisha ombi kwa Serikali ili kuwapatia wananchi msaada wa haraka, ambapo hadi sasa serikali imeanza kuchukua hatua za kutatua changamoto hizo, jambo lililowaletea unafuu wananchi waliokumbwa na janga hilo.Aidha, Dkt. Tulia ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa usikivu wake na ushirikiano mkubwa katika kushughulikia majanga mbalimbali yanayowakumba Wananchi nchini.Vilevile, amewashukuru wananchi wote waliojitokeza kushiriki zoezi la usafi kwa pamoja, na kuwasisitiza kuendelea kushirikiana, kujitolea, na kudumisha mshikamano kila inapojitokeza changamoto katika jamii ili kujenga mazingira salama na yenye ustawi kwa wote.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment