Madereva wanaoendesha Magari yanayohusika na ubebaji wa madini ya ujenzi kama kokoto, mchanga na mengineyo wamepewa elimu ya kufunika madini hayo wanapoingia barabarani ili kuepusha ajali.Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewaeleza Madereva kuwa endapo wakibeba madini hayo bila kuyafunika Kisha kuingia barabarani wanaweza kusababisha madhara Kwa watumiaji wengine wa barabara endapo madini hayo yatadondoka au kupeperushwa na upepo Kisha kusababisha uharibifu wa vyombo vingine vya moto pia madhara Kwa Kwa watembea Kwa miguu.Sajenti Ndimila amewataka madereva hao kutii Sheria bila shuruti na kuwa mabalozi wa usalama barabarani Kwa kuwaelimisha na madereva wengine ili kuzuia ajali za mara Kwa mara.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment