Lydia Lugakila, Misalaba Media MbeyaSpika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Jimbo la Uyole Dkt. Tulia Ackson, ameshiriki ibada ya mazishi ya aliyekuwa dereva wa bodaboda katika Kata ya Nsalaga, Mtaa wa Itezi Mashariki.Tukio hilo limefanyika Januari 4, 2026 ambapo Dkt. Tulia ametoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wanachama wote wa bodaboda kwa msiba mkubwa uliowakumba kufuatia kuondokewa na mwenzao.Aidha, Dkt.Tulia amewahimiza madereva wa bodaboda kuwa waangalifu zaidi wanapokuwa barabarani wakitekeleza shughuli zao za kujipatia kipato kwa ajili ya familia zao.Hata hivyo amewakumbusha kuwa wanabeba dhamana kubwa, kwani wanategemewa na watu wengi wakiwemo wake zao, watoto, wazazi pamoja na ndugu wengine wanaotegemea maisha yao kupitia kazi hiyo.


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment