Na Lydia Lugakila, Misalaba Media MbeyaLeo, Januari 10, 2026, Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Uyole, Spika Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, amepokelewa kwa kishindo na wananchi wa Jimbo la Uyole alipowasili katika Uwanja wa Shule ya Msingi Hasanga.Dkt. Tulia alikuwa katika ziara hiyo kwa ajili ya kugawa vifaa vya shule kwa wanafunzi wa shule za msingi waliopo katika jimbo hilo. Kupitia Taasisi ya Tulia Trust, ametoa msaada wa sare za shule na daftari kwa wanafunzi elfu tatu (3,000) wenye uhitaji zaidi kutoka kata 13 za Jimbo la Uyole.Hatua hiyo inalenga kuwasaidia wanafunzi hao kupata mazingira bora ya kujifunzia na kuchochea maendeleo ya elimu katika jimbo hilo.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment