" MGOGORO ULIO DUMU ZAIDI YA MIAKA 2O KAPRI POINT DIWANI AUVALIA NJUGA

MGOGORO ULIO DUMU ZAIDI YA MIAKA 2O KAPRI POINT DIWANI AUVALIA NJUGA


Mgogoro baina ya wananchi wa Kapripoint na Kanisa la Waadventista wa Sabato iliyodudumu kwa miaka 20 ameingilia Diwani wa Kata hiyo Frank Chacha kwa kuwataka wote kwenye mgogoro huo kumaliza tofauti zao kwa makubaliano yatakayowafanya wote kuridhiana kwa undugu.

Katika mazungumzo hayo diwani aliliomba kanisa la SDA pamoja na wananchi kuvumilia ili wananchi wengi wajitokeze ili kumaliza Tatizo liliodumu Muda Mrefu. 

Alisema ni dhamira ya serikali ya awamu ya sita kumaliza migogoro yote kwenye jamii ili kuwepo na maelewano yatakayowafanya wananchi kuendelea na Shughuli zao vizuri ili wajiletee maendeleo.

  

Post a Comment

Previous Post Next Post