MISA Tanzania jana tarehe 16 Januari 2026 ilipokea ugeni kutoka Farm Radio International (FRI) kwa lengo la kutambulishana na kujadili maeneo ya ushirikiano wa kimkakati kati ya taasisi hizo mbili.
Katika kikao hicho, FRI ilieleza dhamira yake ya kushirikiana na MISA Tanzania kupitia idara yake mpya ya Just Communication Network (JCN), inayolenga kutoa mafunzo kwa vituo vya redio pamoja na mafunzo ya mtandaoni (online skills trainings) kama sehemu ya mkakati wa kujenga uwezo wa wadau wa mawasiliano.
FRI imebainisha kuwa tayari inafanya kazi kwa karibu na MISA Malawi na kwa sasa inatekeleza miradi yake katika takribani nchi 38 barani Afrika. Kupitia mkutano huo, FRI imeonesha nia ya kupanua wigo wa ushirikiano kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya habari kwa upana zaidi, si watangazaji pekee, jambo linaloendana na dira ya MISA ya kulinda na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari pamoja na maendeleo ya taaluma ya habari.
Aidha, FRI imeeleza kuwa iko katika hatua za uzinduzi wa Just Communication Network, ambapo wanakaribisha uanachama binafsi (individual membership). Miongoni mwa faida za uanachama huo ni kupata fursa mbalimbali za mafunzo na kujengewa uwezo kitaaluma.
Kwa pamoja, MISA Tanzania na Farm Radio International wamekubaliana kuendelea na mazungumzo ya karibu ili kufikia muafaka wa maeneo ya ushirikiano yatakayozalisha manufaa na tija kwa pande zote mbili. MISA Tanzania itaendelea kuwajulisha wanachama wake kadri mazungumzo hayo yatakavyoendelea.
Imetolewa na:
Rhoda Maruma
Makamu Mwenyekiti, MISA Tanzania
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment