" TANESCO YATOA ELIMU YA ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME MADINGA

TANESCO YATOA ELIMU YA ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME MADINGA

Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaMaafisa wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  wamekutana na wananchi wa Kijiji cha kitandililo  kilichopo Halmashauri ya njombe kupitia mkutano maalum uliolenga kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulinda na kutunza miundombinu ya umeme inayopita katika maeneo yao.Mkutano huo umefanyika kufuatia kubainika kwa changamoto ya uvunjifu wa taratibu za usalama pamoja na uharibifu wa miundombinu ya usafirishaji umeme katika maeneo mbalimbali yanayopitiwa na njia za kusafirisha umeme, hali inayohatarisha usalama wa wananchi na mali zao pamoja na kusababisha athari kwa upatikanaji wa huduma ya umeme.Akizungumza Msimamizi wa Njia za Usafirishaji Umeme Mkoa wa Ruvuma na Njombe, Mhandisi Liberatus Juma, amesema kuwa kiwango kikubwa cha umeme kinachosafirishwa kupitia njia hizo kinahitaji utii wa sheria na taratibu za usalama .Aidha amewasistiza kuwa maeneo hayo hayaruhusiwi kufanyika kwa shughuli yeyote ya kibinadamu kama kilimo,makazi, biashara na ufungaji kwani kutokufanya hivo kunaweza kuathiri usafirishaji wa umeme kutokana na uharibifu utakaotokeaKwa upende wake,Afisa Mahusiano na huduma kwa wateja Mkoa wa Njombe lucy mtani amesema kuwa jukumu la kulinda miundombinu ya umeme ni la kila mwananchi, akisisitiza kuwa ushiriki wa jamii katika kulinda miundombinu hiyo ni msingi muhimu wa kuhakikisha usalama wa maisha ya watu na uendelevu wa shughuli za kijamii na kiuchumi.Pia amewataka kuweza kutoa taarifa katika shirika endapo wanaona kuna uharibifu kwa kutumia vyanzo rasmi vya mawasiliano vya shirika ili kuweza kusaidiana katika kutunza miundombinu ya usafirishaji

  

Post a Comment

Previous Post Next Post