
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limekanusha taarifa inayosambaa katika mtandao wa kijamii ikieleza kuwa nyumba ya kiongozi wa Polisi Mkoani humo imechomwa moto.
Akitoa taarifa hiyo leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema Jeshi hilo linaendelea kuwasiliana na mamlaka zinazosimamia vyombo vya habari na zile zinazo husika na ulinzi wa taarifa binafsi kwa hatua zaidi za kisheria.
Aidha, ametoa wito na onyo kwa baadhi ya watu wenye tabia za kuandaa na kusambaza taarifa za uongo, kupandikiza chuki na kuchonganisha jamii kuacha kufanya hivyo kwani ni kinyume na sheria.
Sambamba na hilo amebainisha kuwa watu wanaosambaza taarifa kama hizo hawanufaishi jamii na wala haziwanufaishi hata wao wenyewe.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment