Leo Jumapili Januari 18, 2026, kikundi cha SHY TALENT
FILMS kimeendelea na mazoezi ya utayari wa kutengeneza filamu na tamthilia,
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kazi za sanaa zenye lengo la kuelimisha na
kuibua vipaji vya vijana katika Manispaa ya Shinyanga.
Mazoezi hayo yamelenga
kujenga uelewa wa sanaa, kuimarisha uwezo wa uigizaji, ushirikiano wa kikundi
na maandalizi ya kazi zitakazogusa masuala halisi ya kijamii ambapo washiriki
wameendelea kujifunza kwa vitendo, kubadilishana mawazo na kukuza nidhamu ya kazi
ya sanaa.
SHY TALENT FILMS ni
kikundi cha sanaa kilichoanzishwa na Misalaba Media, chombo cha habari cha
mtandaoni kilichosajiliwa kisheria, kinachotumia sanaa kama nyenzo ya
kuelimisha, kuhamasisha na kujenga jamii.
Kwa taarifa zaidi, tembelea ukurasa wao wa Instagram: SHY TALENT FILMS.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment