" TANZANIA YATOLEWA AFCON 2025

TANZANIA YATOLEWA AFCON 2025






Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Morocco imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya Tanzania katika mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa, Januari 4, 2026, nchini Morocco.

Bao pekee la Morocco lilifungwa dakika ya 64 na mchezaji Brahim Díaz, jambo lililowawezesha kusonga mbele katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Kwa upande wa Tanzania, ni mara ya kwanza katika historia yake kufika hatua ya 16 ya michuano ya AFCON tangu kuanzishwa kwake.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post