" VIGOGO 8 KUMINYANA ROBO FAINALI AFCON 2025

VIGOGO 8 KUMINYANA ROBO FAINALI AFCON 2025




Jumla ya mataifa nane yamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 inayoendelea kupigwa nchini Morocco.

Michezo ya robo fainali itaanza kuchezwa Januari 9, 2025, ambapo Mali itachuana vikali na Senegal, huku wenyeji wa mashindano hayo, Morocco, wakivaana na Cameroon.

Ratiba itaendelea Januari 10, 2025 kwa michezo miwili mingine ya robo fainali, ambapo Algeria watamenyana na Nigeria, huku Misri (Egypt) wakiwakabili mabingwa wa watetezi wa kombe hilo, Côte d’Ivoire. Washindi wa michezo hiyo watainga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Post a Comment

Previous Post Next Post