Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Mbeya, Bi Edina Mwaigomole akizungumza.Na Lydia Lugakila-Misalaba Media,MbeyaMwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Mbeya, Bi Edina Mwaigomole, amewataka viongozi wanawake kuwa waangalifu na matumizi ya mitandao ya kijamii, akisisitiza kuepuka vitendo vinavyoweza kudhalilisha viongozi au kuchochea migogoro kwa lengo la kujipatia kipato kupitia mitandao hiyo.Bi Mwaigomole ametoa wito huo Januari 28, 2026, wakati wa semina elekezi kwa viongozi wanawake wa CCM Mkoa wa Mbeya, iliyofanyika katika ofisi za CCM Mkoa.Semina hiyo iliwahusisha wenyeviti na makatibu wa UWT wa wilaya, pamoja na madiwani wa viti maalum kutoka wilaya za Kyela, Chunya, Mbeya Vijijini, Rungwe, Busokelo, Mbalali na Mbeya Mjini.Amesema viongozi wanawake wana wajibu wa kuwa walinzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutokuruhusu kutumika au kuchochea kauli hasi mitandaoni, akieleza kuwa Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kupigania amani na maendeleo ya taifa. Aliongeza kuwa, pale amani inapovurugika, waathirika wakubwa huwa ni wanawake, watoto na vijana.Aidha, amewasisitiza viongozi hao kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za chama, pamoja na kutekeleza Ilani ya CCM kwa ufanisi ili kurahisisha majukumu yao ya kila siku ya kiuongozi.Bi Mwaigomole pia amewataka viongozi wanawake kujenga utamaduni wa kushiriki kikamilifu vikao vya halmashauri, kusoma na kuelewa makabrasha ya vikao ili kuepuka kuonekana kama wameingia kwenye nafasi za uongozi kwa bahati mbaya. Vilevile amewahimiza kushughulikia changamoto za makundi maalum yakiwemo walemavu, pamoja na wananchi wa kawaida.Kupitia semina hiyo, washiriki walipata elimu kuhusu Bima ya Afya kwa Wote, nafasi ya uongozi na watendaji wa UWT, michango ya asilimia 10 kwa madiwani wa viti maalum, uhai wa CCM na UWT, pamoja na maandalizi ya maadhimisho ya miaka 49 ya CCM. Elimu hiyo ilitolewa pia na Afisa Mwanachama Mwandamizi, Bi Anatolia Lusasi, ambaye aliwahimiza viongozi hao kutoa elimu kwa jamii juu ya bima ya afya kwa wote, ikiwa ni dira na agizo la Serikali kwa utekelezaji wa haraka.Kwa upande wake, Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya, Bi Agness Bashemu, amewataka madiwani kuendelea kuhamasisha jamii kujiunga na bima ya afya kwa wote, akibainisha kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi pindi wanapougua.
Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya, Bi Agness Bashemu, akizungumza.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment