" ZAKAYO SHUSHU AZINDUA TUZO ZA KUWATHAMINI WATENGENEZA MAUDHUI

ZAKAYO SHUSHU AZINDUA TUZO ZA KUWATHAMINI WATENGENEZA MAUDHUI

Na Mwandishi wetu, Misalaba Media‎Mradi wa Tanzania Creators Awards umezinduliwa rasmi kwa lengo la kutambua, kuthamini na kuhamasisha mchango wa watengeneza maudhui (content creators) wanaotoa athari chanya kwa jamii ya Watanzania.‎Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa mradi huo, Zakayo Shushu, amesema kuwa katika kipindi cha sasa watengeneza maudhui wamekuwa na nafasi kubwa katika kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha jamii, sambamba na kuchangia ukuaji wa uchumi kupitia uundaji wa ajira na utangazaji wa biashara mbalimbali.‎Zakayo amesema kuwa maendeleo ya teknolojia na mitandao ya kijamii yameifanya sekta ya uundaji wa maudhui kuwa ajira kamili kwa vijana wengi, hali inayohitaji kuthaminiwa na kuungwa mkono rasmi.‎“Tanzania Creators Awards imelenga kuwapa motisha watengeneza maudhui kwa kuzingatia thamani, ubunifu na athari ya kazi zao katika kuleta mabadiliko chanya kwa jamii. Tuzo hizi zitakuwa jukwaa la kutambua juhudi zao na kuwahamasisha kuendelea kutoa maudhui yenye tija,” amesema Zakayo.‎Ameongeza kuwa tuzo hizo pia zinalenga kukuza maadili, uzalendo na ubunifu miongoni mwa watengeneza maudhui, ili kuhakikisha maudhui yanayotengenezwa yanazingatia maslahi mapana ya Taifa.‎Kwa mujibu wa waandaaji, Tanzania Creators Awards zinatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya ubunifu, wakiwemo watengeneza maudhui, makampuni, wadhamini na taasisi za serikali, ili kwa pamoja kuimarisha tasnia hiyo inayokua kwa kasi nchini.

Post a Comment

Previous Post Next Post