" Bi GROLIA IPOPO AELEZA FAIDA ZA SEMINA YA UWT MBEYA

Bi GROLIA IPOPO AELEZA FAIDA ZA SEMINA YA UWT MBEYA


 

Na Lydia Lugakila .Mbeya

‎Diwani wa kata ya Iwambi jijini Mbeya Mhe, Grolia Ipopo Mwamajemba, maarufu Mchina, amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Mbeya kupitia Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UWT) kwa kuwajengea uwezo viongozi wa wanawake kupitia semina maalum ya uongozi.

‎Bi, Grolia Ipopo ametoa pongezi hizo baada ya kufanyika kwa semina ya uongozi kwa viongozi watendaji wa UWT mkoani humo, iliyolenga kuwajengea uwezo pamoja na kuwakumbusha misingi, kanuni na sifa za kiongozi bora ndani ya jamii.

‎Bi Ipopo amesema kupitia semina hiyo wamejifunza kwa kina maana halisi ya uongozi, maadili ya kiongozi bora pamoja na taratibu sahihi za kuongoza jamii kwa ufanisi.

‎Diwani huyo ameongeza kuwa semina hiyo imekuwa na umuhimu mkubwa kwa madiwani na viongozi wanaowahudumia wananchi, kwani imewasaidia kujifunza namna bora ya kuishi na kushirikiana na wananchi kwa upendo.

‎"tumepata mafunzo kuhusu mahusiano mazuri ndani ya familia na katika jamii kwa ujumla uvumilivu, busara na kuwatumikia wananchi kwa moyo wa kujitolea ni nguzo kuu za uongozi bora na tutajitahidi kutenda hayo"alisema diwani huyo.

‎Aidha, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuanzisha na kuboresha bima ya afya kwa wote kwa gharama nafuu, ambapo watu sita watahudumiwa kwa shilingi laki moja na hamsini (150,000 )ambapo diwani huyo ameeleza kufurahishwa kwake kuona makundi maalum, wakiwemo watu wenye ulemavu pamoja na wanufaika wa TASAF, wakienda kupata huduma za afya kwa urahisi na ufanisi zaidi pamoja na Wananchi wengine.

Post a Comment

Previous Post Next Post