Na: Belnardo Costantine, Misalaba Media
Mku wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)Jenerali Jacob John Mkunda amefunga rasmi mafunzo ya askari wapya katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi "RTS" Kihangaiko Msata mkoani Pwani.
Aidha Jenerali Mkunda amewataka askari wapya kukiishi na kuzingatia kiapo cha utii wakati wote watakapokuwa wakitekeleza majukumu yao sehemu mbalimbali watakayopangiwa, huku akisisitiza kuchukuliwa hatua kwa askari watakaokwenda kinyume na kiapo chao.
Askari hao wameaswa kuendelea kukiishi kiapo cha kijeshi kitakacho waweka mbali na mambo ambayo ni kinyume na taratibu za kijeshi ikiwemo kutojihusisha na siasa, matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, matumizi ya dawa za kulevya, michezo ya kamari na kuepuka madeni yasiyo na tija.
Hatahivyo Mkuu wa Majeshi amewataka askari hao kutunza afya zao na kuzingatia lishe bora wakati wote wanapotekeleza majukumu yao.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment