Mashindano ya Wailes Super Cup yameendelea kuthibitisha umuhimu wake kama jukwaa la kuibua vipaji vya soka kwa vijana baada ya kutangaza rasmi kuwa yatatoa fursa kwa wachezaji bora kujiunga na ENJOY SOKA ACADEMY inayomilikiwa na nyota wa zamani wa Taifa Stars, Mrisho Ngasa. Academy hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam inalenga kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana katika soka la ushindani.
Taarifa hiyo imebainika wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo uliofanyika katika Kata ya Lukanzauti, Wilaya ya Mbinga, ambapo Mrisho Ngasa alikuwa mgeni rasmi.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Ngasa aliyewahi kuzichezea klabu kubwa nchini ikiwemo Yanga SC, Simba SC na Azam FC, amewataka wachezaji kushiriki mashindano hayo kwa bidii na kuonesha uwezo wao halisi. Amesema Wailes Super Cup ni fursa adimu kwa vijana wenye ndoto ya kufika mbali zaidi katika soka, hivyo wanapaswa kuitumia vyema.
Ngasa ameongeza kuwa wachezaji watakaoonesha kiwango cha juu kupitia mashindano hayo watapata nafasi ya kujiunga na ENJOY SOKA ACADEMY, hatua itakayowawezesha kupata mafunzo bora pamoja na kupata exposure nje ya Mkoa wa Ruvuma. Amehimiza nidhamu, kujituma na kujitolea kuwa silaha muhimu katika kufanikisha ndoto za soka.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Wailes Company Limited, ndugu Frank Ndunguru, amesema lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kuhakikisha vipaji vilivyopo kwenye jamii vinaibuliwa na kuendelezwa. Ameeleza kuwa michezo ni ajira kama ajira nyingine, hivyo jamii inapaswa kuupa uzito unaostahili ili kuwasaidia vijana kujenga maisha yao kupitia soka.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment