" CRDB GEITA YATOA MAFUNZO YA MATUMIZI YA INTERNET BENKI KWA WATEJA WA TAASISI

CRDB GEITA YATOA MAFUNZO YA MATUMIZI YA INTERNET BENKI KWA WATEJA WA TAASISI










Benki ya CRDB Bank Tawi la Geita imetoa mafunzo kwa wateja wake wa taasisi mbalimbali kuhusu matumizi ya mfumo wa Internet Benki, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kurahisisha huduma na kupunguza msongamano wa wateja katika matawi.

Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wateja ili waweze kufanya miamala yao nje ya tawi kwa urahisi, ikiwemo kufanya malipo mbalimbali bila usumbufu.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Geita, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Lucy Beda, amesema kuwa matumizi ya Internet Benki yatawasaidia watumiaji kuokoa muda na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kifedha.

Kwa upande wake, Meneja wa Kanda wa benki hiyo, Anselm Mwenda, amesema maboresho yaliyofanyika kwenye mfumo huo yameongeza ufanisi mkubwa katika utumaji wa miamala, ambapo sasa mteja anaweza kutuma fedha kwa watu wengi kwa wakati mmoja bila kukwama.

Ameeleza kuwa licha ya huduma hiyo kuwapo kwa muda mrefu, bado baadhi ya wateja hawakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu namna bora ya kuitumia, hali iliyochochea benki hiyo kutoa mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameeleza kufurahishwa na huduma ya Internet Benki, wakisema imewasaidia kuokoa muda na gharama, tofauti na awali ambapo walilazimika kubeba nyaraka mbalimbali kufika benki kwa ajili ya kufanya malipo, ikiwemo mishahara ya wafanyakazi.

 

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post