" KATIBU JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA MPANDA AFANYA KIKAO NA MAKATIBU WA KATA

KATIBU JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA MPANDA AFANYA KIKAO NA MAKATIBU WA KATA



Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda, Ndugu Jimotoli Jilala Maduka, leo Februari 23, 2026 amefanya kikao na makatibu wa Jumuiya ya Wazazi ngazi ya kata wilayani humo kwa lengo la kuwapatia maelekezo ya kiutendaji katika utekelezaji wa majukumu yao.

Katika kikao hicho kilichowakutanisha makatibu wa kata, Maduka amewasisitiza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi wa kutosha, ikiwemo kuhimiza uhai wa Jumuiya kwa kuongeza wanachama wapya na kuhakikisha ada za uanachama zinalipwa kwa wakati.

Aidha, amewaelekeza makatibu wote kupita katika kila tawi ndani ya kata zao kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zilizopo katika matawi, hatua ambayo inalenga kuimarisha mshikamano na ufanisi wa Jumuiya ngazi ya chini.

Makatibu wa Jumuiya ya Wazazi kata wilayani Mpanda wamekubali kuyatekeleza maelekezo hayo kwa mujibu wa miongozo ya Jumuiya na chama, huku wakiahidi kuongeza juhudi katika kusimamia shughuli za Jumuiya katika maeneo yao.Kadhalika, Maduka amesisitiza umuhimu wa kuzingatia vikao vya kikanuni ili kuhakikisha majukumu yanatekelezwa kwa ufanisi zaidi na kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.

Akifunga kikao hicho, Katibu huyo amehimiza umoja na mshikamano miongoni mwa makatibu wa kata ili kuendelea kuimarisha Jumuiya na chama kwa ujumla.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda, Ndugu Jimotoli Jilala Maduka, akiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kikao.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda, Ndugu Jimotoli Jilala Maduka, akiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kikao.

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


 

Post a Comment

Previous Post Next Post