Na Lydia Lugakila, Misalaba Media MbeyaHospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) imeendelea kuandika historia mpya katika sekta ya afya baada ya kusaini makubaliano ya ushirikiano na Shirika la CURE Neuro, lenye makao makuu Michigan, Marekani.Ushirikiano huo unalenga kuimarisha huduma za matibabu kwa watoto wenye tatizo la vichwa kujaa maji (Hydrocephalus) na mgongo wazi (Spina Bifida), huku ukiiweka hospitali katika ramani ya kimataifa ya utoaji wa huduma za kibingwa.Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji, alisema kuwa dira ya hospitali ni kuwa kituo kinara cha utoaji wa huduma za kibingwa na kibobezi chenye viwango vya kimataifa. Aidha, amelishukuru Shirika la CURE Neuro kwa kuhakikisha Watanzania na wananchi kutoka nchi jirani wenye changamoto hizo wanapatiwa huduma bora na salama bila ubaguzi.Kupitia makubaliano hayo, hospitali itanufaika na teknolojia na vifaa vya kisasa vinavyotumika katika hospitali za kimataifa, ikiwemo Hospitali ya Watoto inayoshughulika na matatizo ya ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu, inayojulikana kama CURE Neuro iliyoko Mbale, Uganda, chini ya shirika hilo. Hatua hii itaimarisha ubora, usalama na ufanisi wa huduma kwa watoto wa Tanzania na nchi jirani, bila kulazimika kusafiri umbali mrefu, na pia itasaidia kujenga uwezo wa wataalamu kupitia mafunzo na kubadilishana uzoefu na wataalamu wa kimataifa.Naye Joshua Menya, Meneja wa Mradi wa CURE Neuro chini ya CURE International (Africa Division), ameshukuru Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kushirikiana nao, akisema kuwa makubaliano hayo yatafungua ukurasa mpya na kuonyesha imani kubwa ya CURE Neuro kwa uwezo wa wataalamu wa hospitali hiyo. Aliongeza kuwa kwa pamoja, watahakikisha watoto wengi zaidi wanapata huduma bora kwa wakati. Mbali na kuboresha huduma kwa wananchi wa Tanzania, hatua hiyo pia itachangia ukuaji wa utalii wa matibabu (medical tourism) katika Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment