Na Fabius Clavery, Misalaba Media-Kagera.
Mkuu mpya wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Ramadhani Kido, amewasili rasmi mkoani humo Februari 11, 2026, tayari kuanza majukumu yake ya kuwatumikia wananchi na kusimamia shughuli za maendeleo. Ujio wake unaashiria mwanzo wa sura mpya ya uongozi katika mkoa huo, huku wananchi wakitarajia kuona kasi mpya ya utekelezaji wa miradi na huduma za kijamii.
Kanali Kido anatarajiwa kukabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Hajath Fatma Mwassa, katika hafla ya makabidhiano itakayofanyika Ijumaa, Februari 13, 2026, kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Kiongozi huyo aliteuliwa rasmi Februari 6, 2026 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kisha kuapishwa Februari 9, 2026, akipewa dhamana ya kuongoza na kuratibu shughuli za Serikali katika Mkoa wa Kagera.
Akiwa na jukumu la kusimamia maendeleo ya mkoa huo, Kanali Kido anatarajiwa kuimarisha sekta muhimu ikiwemo miundombinu, afya, elimu na uwekezaji, sambamba na kudumisha amani na usalama. Wananchi wa Kagera sasa wanaelekeza macho yao kwa uongozi wake mpya wakitarajia matokeo chanya yatakayochochea ustawi wa kijamii na kiuchumi wa mkoa wao.
HABARI PICHA.
Kanali Yahya Ramadhani Kido (kulia) akitembea na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima, muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba kwa ajili ya kuanza rasmi majukumu yake.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Ramadhani Kido, akisalimu na kusalimiana na viongozi mbalimbali wa ulinzi na usalama pamoja na viongozi wa Serikali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba mkoani Kagera.
Kanali Yahya Ramadhani Kido akisalimiana na Katibu Tawala Msaidizi, Divisheni ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Isaya Tendega, wakati wa mapokezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment