Baraza la
wazazi Mkoa wa Shinyanga limefanya kikao chake cha kawaida cha baraza la
kufunga mwaka 2025 tarehe 12/02/2026, kikao hicho ambacho kilikuwa kinaongozwa
na mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Shinyanga ndugu John Siagi.
Katika kikao hicho ndugu John Siagi amewaomba wajumbe
wa Baraza kuwa na umoja na mshikamano wa dhati katika kuendeleza na kuimarisha
jumuiya ya wazazi mkoa wa shinyanga, huku akiwapongeza wajumbe kwa ushirikiano
wao katika utekelezaji wa majukumu ya chama kwa mwaka mzima wa 2025 ambapo
mwenyekiti huyo ametumia nafasi hiyo kuwasalimia wajumbe na kuwatakia heri ya
mwaka mpya 2026.
Ndugu John Siagi mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa
wa Shinyanga ametumia wasaa kuzungumzia uchaguzi mkuu wa 2025, baraza la wazazi
mkoa wa shinyanga linakipongeza chama cha mapinduzi kwa ushindi mkubwa katika
ngazi zote za uongozi ikiwemo Udiwani wa Kata, Udiwani viti maalumu, Ubunge,
Ubunge viti maalumu na Urais ambapo jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga
limeeleza kuridhishwa na matokeo hayo na kuishukuru CCM kwa kuendelea kushika
dola.

Ndugu Regina Ndulu katibu wa jumuiya ya wazazi mkoa shinyanga ameeleza kuwa jumuiya ya wazazi mkoa wa shinyanga inaendelea kuwa imara na iko mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yake ya chama kwa ufanisi na weledi, akisisitiza umuhimu wa kila mjumbe kutimiza wajibu wake ndani ya jumuiya na CCM kwa ujumla.
Ndugu Regina ameendelea kusisitiza wajumbe kuimarisha
umoja na mshikamano, pamoja na kushiriki kikamilifu katika kazi za jumuiya ya
wazazi na chama cha mapinduzi ili kuongeza ufasini wa utendaji kazi kwa
uanachama wote waliopo kwenye nafasi mbalimbali za chama. Katika hatua nyingine
jumuiya ya wazazi Mkoa wa Shinyanga inatoa shukrani za dhati kwa Dkt. Samia Suluhu
Hassan, Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa
kuibuka na ushindi wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa 2025 na kutamka wazi
kuwa “HONGERA SANA”
Kikao hicho cha baraza pia kimejadili kuimarisha uhai wa jumuiya ya wazazi, ambapo Ndugu Regina Katibu wa wazazi mkoa wa
Shinyanga amewahimiza wajumbe kuendelea kulipia ada za wanachama, kutoa
hamasa ya uandikishaji au usajili wa
wanachama wapya na kuendelea kutoa elimu ngazi za matawi, mashina, kata, wilaya
na mkoa ili kuongeza idadi ya wanachama kupitia jumuiya ya wazazi na chama cha
mapinduzi kwa ujumla.
Aidha, jumuiya ya wazazi mkoa wa shinyanga imeeleza
kuridhishwa na mafanikio ya kisiasa yaliyopatikana katika uchaguzi mkuu wa 2025,
ambapo jumuiya ya wazazi imeweza kupata Madiwani wanao tokana na jumuiya ya
wazazi wengi ambao sisi kama jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga ni mchango
mkubwa sana kwa CCM na faraja kubwa sana
na hii ni kutokana na elimu, hamasa ya kuhamasisha wanachama kutia nia ya
kugombea nafasi walizokuwa wanahitaji kuchukua fomu kwa ajili ya nafasi
mbalimbali zilizokuwa zimetangazwa kama vile udiwani, ubunge na urais.

Ndugu, Edwin Peter Nyakanyenge mjumbe wa baraza kuu wazazi Taifa anayetokana na mkoa wa Shinyanga pia mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi Taifa ameshiriki kikamilifu baraza la funga mwaka 2025 mkoa wa Shinyanga kwa kuwahimiza wajumbe wote wa baraza kwa nafasi zao kuwa wenye umoja na mshikamano wa dhati katika kutekeleza majukumu ya kila mjumbe na kwa nafasi yake aliyonayo kuhakikisha jumuiya ya wazazi mkoa wa shinyanga inafanya kazi kwa ufanisi, weledi, upendo, amani, utulivu na mshikamano wa hali ya juu kuhakikisha jumuiya ya wazazi inasonga mbele bila kukwama au kukwamishwa na mtu asiye tekeleza majukumu yake.

Ndugu Richard Masele
katibu wa itikadi na uenezi CCM Mkoa wa Shinyanga ameshiriki kwenye baraza
la wazazi Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya
katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga ndugu Odilia akisisitiza wajumbe wote wa baraza
na wanachama kwa ujumla kila mjumbe kutambua majukumu yake na ametumia wasaa
kuwakumbusha wajumbe kuwa na umoja na mshikamano katika nafasi kwa kila mmoja aliyonayo
aitumie kwa ufasaha na kwa weledi wa kuridhisha. Sambamba na hayo ndugu Richard
Masele wamewasisitiza wajumbe wa baraza na wanachama kwa ujumla kuendelea kuvaa sale za chama bila woga.

Ndugu Jimotoli Jilala Maduka katibu wa Jumuiya ya
wazazi CCM wilaya ya Mpanda Mkoa
wa Katavi leo tarehe 12/02/2026 asalimia baraza la wazazi mkoa wa Shinyanga kwa
kuwashukuru na kuwapongeza viongozi wote wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Shinyanga na kuwatakia heri ya mwaka mpya 2026 ambapo amewashukuru wajumbe wote kwa ujumla
kupitia baraza hilo la funga mwaka 2025.
Kutokana na
baraza hili la jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga uongozi wa kamati ya
utekelezaji wazazi mkoa wa Shinyanga umeshukuru kwa umoja na mshikamano,
mchango, mawazo, ushauri pamoja na mambo mengine kwa kila mjumbe kwa kushiriki baraza
hili la tarehe 12/02/2026.
Mwisho wa kikao, ndugu John Siagi mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga amelifunga rasmi
baraza la kufunga mwaka 2025 kwa kuwashukuru wajumbe wote kwa mawazo,
mchango,maoni, mapendekezo, ushauri na kwa kuunga mkono juhudi, bidii pamoja na
mipango na mikakati ya jumuiya hususani
katika utekelezaji wa miradi ya nyumba za watumishi wa jumuiya za wilaya
na mkoa, miradi ya shule na masuala mengine yaliyojadiliwa katika kikao hicho
cha baraza la tarehe 12/02/2026 na baada ya hapo mwenyekiti akafunga kikao
mpaka siku nyingine.
Sambamba na hayo yote yaliyojadiliwa kwenye kikao jumuiya ya wazazi Mkoa wa Shinyanga kupitia baraza hilo la funga Mwaka imenufaika na mafunzo ya ufugaji wa Nguruwe.
Ndugu Richard Masele, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.
Ndugu Regina Ndulu, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga.
Ndugu Edwin Peter Nyakanyenge, Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Taifa.
Ndugu Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment