Na, Egidia Vedasto,
Misalaba Media.
Kampuni ya usafirishaji ya mabasi ya Loliondo coach inayopatikana Jijini Arusha yamewahakikishia abiria wake usalama wa kutosha pamoja na huduma bora kila wakati wawapo safarini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Chilia Kimambo baada ya kununuliwa kwa mkupuo mabasi mapya matatu ishara hiyo ikionyesha hatua kubwa ya kibiashara na uhakika wa usafiri kwa watumiaji wake.
Aidha amewaomba wateja kuendelea kuiamini kampuni hiyo na kuwaahidi huduma bora daima.
"Nawashukuru sana wateja wetu, nakiri kuwa mafanikio haya yametokana na upendo na utayari wenu kwa kutumia mabasi yetu kwa miaka mingi" amesema Kimambo.
Mmoja wa wateja Lucy Godfrey anayetumia mabasi hayo mara nyingi kutoka Arusha kwenda Musoma, amepongeza kampuni hiyo kwa hatua kubwa ya mafanikio.
Amesema kuwa huduma zao ni nzuri na wana lugha nzuri wanapowasiliana na wateja wao.
Kampuni ya mabasi ya Loliondo Coach ni kongwe na inayoaminika na wengi. Hufanya safari zake kuanzia Moshi kwenda Mwanza hadi Musoma.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment