Na Lydia Lugakila- Misalaba MediaMbeyaMfanyabiashara maarufu jijini Mbeya, Mdope Michael Sanga, ameishauri Serikali kuona umuhimu wa kuongeza matukio makubwa pamoja na kuhamasisha uwekezaji wa viwanda ili kuchochea ujio wa wageni na kukuza mzunguko wa fedha mkoani Mbeya.Akizungumza na Misalaba Media Februari 25, 2026 jijini Mbeya, Mdope amesema kuongezeka kwa matukio na viwanda kutasaidia kuvutia wageni wapya kutoka maeneo mbalimbali, hali itakayoongeza uhitaji wa huduma za malazi, chakula na burudani.Ameeleza kuwa kwa sasa bado kuna changamoto ya hoteli kukosa wateja wa kutosha, ambapo baadhi ya hoteli zenye uwezo wa vyumba 30 hulaza wageni wasiopungua 15 tu kwa wakati mmoja, jambo linaloathiri mapato na ukuaji wa sekta hiyo.Ameongeza kuwa ujio wa viwanda utaleta wageni wa kikazi, wawekezaji na wataalamu mbalimbali watakaohitaji huduma bora za malazi na hivyo kuinua sekta ya hoteli jijini Mbeya.Hoteli ya kisasa ya Ndope Idde Hotel, inayopatikana eneo la Mama John Bus Stop jijini Mbeya, imeendelea kufanya vizuri kwa kutoa huduma bora kwa wateja wake wa ndani na nje ya mkoa huo.Kwa mujibu wa Mdope, hoteli hiyo inaendeshwa na wataalamu waliobobea katika masuala ya ukarimu, huku ikiwa na ulinzi wa kutosha saa 24 ili kuhakikisha usalama wa wageni na mali zao.Amebainisha kuwa hoteli hiyo ina vyumba zaidi ya 30 vyenye viwango na bei tofauti, maji safi na salama, huduma ya intaneti ya bure, maegesho ya magari, pamoja na ukumbi wa mikutano unaoweza kubeba watu kati ya 150 hadi 200.Mbali na hilo, hoteli hiyo pia inatoa huduma bora za chakula na vinywaji, ikiwa na baa maalum ya VIP, sehemu nzuri ya mapumziko, kifungua kinywa pamoja na matunda kwa wageni wake.Katika hatua nyingine, hoteli hiyo inatarajia kuanzisha rasmi huduma ya kumfuata na kumrudisha mteja katika uwanja wa ndege endapo atafanya mawasiliano mapema.Akizungumzia uboreshaji wa huduma hiyo mpya inayotarajiwa katika hoteli hiyo, Meneja Mkuu Joseph Kariuki amesema kuwa mteja atakapowasili atafuatwa na usafiri maalum wa hoteli na kurudishwa uwanja wa ndege atakapokuwa anasafiri. Ameongeza kuwa gharama za shughuli nyingine za mteja akiwa mjini zitabaki kuwa jukumu lake binafsi.Kwa mujibu wa Kariuki, lengo la maboresho hayo ni kuhakikisha wageni wanapata huduma ya kisasa yenye viwango vinavyokidhi ushindani wa sekta ya hoteli nchini.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment