Na Mapuli Kitina Misalaba
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Mongella, amesema chama hicho kitaendelea
kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Ilani ya CCM ili kuhakikisha wananchi
wananufaika na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.
Mongella ameyasema hayo
leo Februari Mosi, 2026, wakati wa ziara yake katika Jimbo la Itwangi mkoani
Shinyanga, ambapo ametembelea maeneo mbalimbali, kusikiliza kero za wananchi
pamoja na kufanya mkutano wa hadhara.
Kabla ya mkutano huo wa
hadhara, Mongella amefanya kikao cha ndani, ambapo katika mkutano wa hadhara
amepokea changamoto zilizowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Itwangi kwa niaba ya
wananchi, huku akiahidi kuzifikisha katika wizara husika ili zishughulikiwe kwa
wakati.
Kwa upande wake, Mbunge
wa Jimbo la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, ametumia fursa hiyo kumshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uamuzi
wa kugawa Jimbo la Solwa na hatimaye kupatikana kwa Jimbo jipya la Itwangi,
hatua aliyosema imeanza kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Amesema ndani ya Jimbo la
Itwangi, utekelezaji wa Ilani ya CCM umeleta mafanikio makubwa ikiwemo kupita
kwa Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaopita katika kata sita, mradi aliousema
umefungua fursa za kiuchumi na kibiashara kwa wananchi wa jimbo hilo.
Aidha, Azza amepongeza
Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuleta miradi mikubwa ya maji safi na salama,
akitaja miradi inayotekelezwa katika kata za Imesela na Bukene chini ya
usimamizi wa RUWASA kwa kushirikiana na Life Water, miradi itakayohudumia
vijiji vyote vilivyopo katika kata hizo.
Ameeleza kuwa Jimbo la
Itwangi lina vijiji 58, ambapo vijiji 14 vina mradi wa maji ya Ziwa Victoria,
vijiji 9 vina visima virefu, huku vijiji 35 bado havijafikiwa na huduma ya
maji, lakini Wizara ya Maji imeahidi kuanza utekelezaji wa miradi katika vijiji
vitano ndani ya siku 100 na kuhakikisha vijiji vyote vinapata maji safi na salama
ndani ya kipindi cha miaka mitano.
Katika sekta ya
miundombinu, Mbunge huyo ameomba Serikali kuboresha barabara ya
Ishinabulandi–Imenya kwa kiwango cha Changalawe pamoja na ujenzi wa madaraja,
akisema hiyo ndiyo barabara muhimu lakini mbovu zaidi ndani ya Jimbo la
Itwangi.
Pia ameomba ujenzi wa barabara ya Didia kwenda Didia
Senta yenye urefu wa takribani kilomita saba kuboreshwa kwa kiwango cha lami ili kuchochea biashara katika miji
ya Didia na Tinde, ambayo imekua kwa kasi kutokana na shughuli za kilimo na
biashara ya mpunga.
Baadhi ya wakazi wa Jimbo
la Itwangi akiwemo Sabina Mwang’onda, Amina Sanga, Mwajuma Masanja na Masanja
Charles, wamekiri kuwepo kwa changamoto hizo, huku wakiongeza kuwa bado kuna
vijiji ambavyo havijafikiwa na huduma ya umeme.
Ziara hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 49 ya Chama cha Mapinduzi (CCM), yanayobebwa na kauli mbiu isemayo “TUMECHAGUA UMOJA NA AMANI KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU.”
John Mongella akisisitiza umuhimu wa CCM kusimamia miradi ya maendeleo kwa wananchi wa Itwangi.
John Mongella akisisitiza umuhimu wa CCM kusimamia miradi ya maendeleo kwa wananchi wa Itwangi.
Kikao cha ndani kikiendelea chini ya uongozi wa John Mongella, wakipanga hatua za kushughulikia masuala ya maendeleo ya Itwangi.
Kikao cha ndani kikiendelea chini ya uongozi wa John Mongella, wakipanga hatua za kushughulikia masuala ya maendeleo ya Itwangi.
Azza Hillal akibainisha miradi mikubwa ya maji, barabara na SGR inayoboreshwa katika jimbo la Itwangi.
Azza Hillal akibainisha miradi mikubwa ya maji, barabara na SGR inayoboreshwa katika jimbo la Itwangi.
Mbunge wa Itwangi, Azza Hillal, akishirikiana na wananchi kueleza kero na matarajio yao kwa wizara husika.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa, akizungumza na wananchi kuhusu maendeleo jimbo la Itwangi.
Wanachama wa CCM na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wakisikiliza viongozi wa chama na kushauriana kuhusu maendeleo ya jimbo.
Wanachama wa CCM na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wakisikiliza viongozi wa chama na kushauriana kuhusu maendeleo ya jimbo.
Mbunge wa Itwangi, Azza Hillal, akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kugawa jimbo jipya la Itwangi.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




















Post a Comment