" SIMBA SC YAENDELEA KUBURUZA MKIA LIGI YA KLABU BINGWA AFRIKA

SIMBA SC YAENDELEA KUBURUZA MKIA LIGI YA KLABU BINGWA AFRIKA






Katika Kundi D, Michuano ya kombe la Klabu Bigwa Afrika , Simba SC inaendelea kuburuza mkia baada ya kukusanya pointi moja pekee katika michezo minne ya msimu wa 2025/26. Matokeo hayo yanazidi kuyeyusha ndoto za Wekundu wa Msimbazi za kutinga hatua inayofuata, wakibaki na mechi mbili tu huku wakiwa na pointi kiduchu.

Kwa hali ilivyo, hesabu hazipo upande wa Simba SC kufuzu hatua ya robo fainali, hasa iwapo Esperance watafanikiwa kupata matokeo chanya katika mchezo wao ujao. Hivyo, matumaini ya Simba SC kwa msimu huu wa 2025/26 yanaonekana kuwa hafifu.

Katika mchezo wa nne uliochezwa Februari 1, 2026 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba SC walilazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Esperance.

Shomari Kapombe aliitanguliza Simba SC dakika ya 39, kabla ya Yusuph Kagoma kuongeza bao la pili dakika ya 45. Hata hivyo, Esperance walifanikiwa kusawazisha kupitia Aboubacar Diakite dakika ya 64 na Kouceilia dakika ya 79.

Kiungo wa Simba SC, Yusuph Kagoma, alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mchezo kutokana na kiwango bora alichokionesha, huku nyota wa Esperance H. Jelassi akikosa nafasi ya kuipatia timu yake bao baada ya kukosa mkwaju wa penalti.


Post a Comment

Previous Post Next Post