Kampuni ya Kitanzania ya Jitegemee Holding Company Limited, inayojihusisha na uchakataji na uuzaji wa makaa ya mawe , imeanzisha mradi wa nishati safi kwa kutumia makaa ya mawe kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali katika utunzaji wa mazingira na upatikanaji wa nishati mbadala.
Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Abbass Ahmed, alipotembelea mgodi wa kampuni hiyo uliopo wilayani Mbinga, kwa lengo la kujionea hali halisi ya uendeshaji wa shughuli za uchimbaji na usindikaji wa makaa ya mawe pamoja na changamoto zinazowakabili katika shughuli zao
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa migodi makaa ya mawe Mkoa wa Ruvuma, Bosco Mabena, amesema licha ya kampuni kujihusisha na uchakataji na uuzaji wa makaa ya mawe, jambo lililomfurahisha zaidi Mkuu wa Mkoa ni hatua ya kampuni kuwekeza katika uchakataji wa nishati safi kwa kutumia mchanganyiko maalumu wa makaa ya mawe.
Mabena ameeleza kuwa mradi huo wa nishati safi unaendana na falsafa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, inayosisitiza matumizi ya nishati mbadala na rafiki kwa mazingira ili kupunguza uharibifu wa mazingira na kulinda rasilimali za asili.
Aidha, kampuni hiyo imeiomba serikali kupitia kwa Mkuu wa Mkoa kuwapatiwa shule mbili zitakazotumika za mfano (shamba darasa), zitakazosaidia kutoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi ya nishati safi, huku akieleza kuwa tayari huduma hiyo imeanza kusambazwa katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brig. Kanali Abbass Ahmed, ameipongeza Jitegemee Holding Company Limited kwa kuanzisha mradi wa nishati safi, amesistiza kuwa hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kasi ya ukataji wa miti na kuchangia katika uhifadhi wa mazingira kwa maendeleo endelevu ya mkoa na taifa kwa ujumla.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment