
TANZANIA imepiga hatua kubwa ya kihistoria baada ya kutajwa kuwa miongoni mwa nchi 45 za mfano bora duniani (Tier 1) katika usimamizi wa masuala ya usalama mtandaoni, huku ikishika nafasi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Usalama Mtandaoni jijini Dodoma, Februari 10, 2026, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari, amesema mafanikio hayo ni kielelezo cha uimara wa mifumo ya nchi katika kulinda watumiaji wa mawasiliano na miundombinu ya kidijitali.
Dkt. Bakari amebainisha kuwa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) limetoa tathmini hiyo baada ya kuridhishwa na jitihada za makusudi zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha nyanja tano muhimu za usalama wa mitandao ambazo ni; kisheria, kiufundi, kitaasisi, ujenzi wa uwezo, na ushirikiano wa kimataifa.
"Kuwa miongoni mwa nchi 45 za mfano duniani kati ya nchi takriban 193 wanachama wa ITU si jambo dogo. Ni matokeo ya uwekezaji mkubwa katika Kituo cha Taifa cha Kusimamia Matukio ya Uhalifu Mtandaoni (TZ-CERT) na ushirikiano wetu na wadau wa usalama nchini na nje ya nchi," alisema Dkt. Bakari.
Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa nafasi hiyo ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati inaimarisha hadhi ya Tanzania kama kitovu salama cha biashara na uwekezaji wa kidijitali. Alisisitiza kuwa usalama wa mtandao ni msingi mkuu wa kukuza uchumi wa kidijitali kwani unajenga imani kwa wananchi na wawekezaji kutumia mifumo ya kielektroniki bila shaka.
Aidha, Dkt. Bakari alitumia fursa hiyo kuwasihi watumiaji wa mtandao nchini kuendelea kuzingatia misingi ya usalama, ikiwemo kutumia nenosiri imara na kutotoa taarifa binafsi kwa watu wasiofahamika, akibainisha kuwa teknolojia inabadilika kwa kasi na inahitaji umakini wa hali ya juu.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment