" YANGA SC YAICHAPA JKT TANZANIA 5-0

YANGA SC YAICHAPA JKT TANZANIA 5-0






Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans Sports Club, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliochezwa leo, Februari 25, 2026, kwenye Dimba la KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Zimbwe Jr dakika ya 7, Depu dakika ya 60, Mudathir dakika ya 63, Dube dakika ya 85, huku bao la tano likifungwa na Khamis dakika ya 89 na kuhitimisha wimbi la ushindi.

Ushindi huo ni sehemu ya ujumbe thabiti kwa wapinzani wao, Simba Sports Club, kabla ya Dabi ya Kariakoo itakayofanyika Jumapili, Machi 1, 2026.

Mashabiki wa Yanga baada ya ushindi huo walionekana wakiimba, “Bado Simba! Bado Simba!” kuelekea mechi ya Dabi ya Kariakoo itakayofanyika Jumapili, Machi 1, 2026, Visiwani Zanzibar.

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post