
DARAJA la Mto Ruhembe, lililoko Mikumi linalounganisha Mji wa Mikumi na eneo la Ifakara limekatika leo alfajiri baada ya kuharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.
Mwandishi wa habari aliyepo eneo la tukio ameshuhudia uharibifu huo wa daraja hilo, ambao umepelekea kukatika kwa mawasiliano ya barabara kati ya Mikumi na Ifakara, njia muhimu inayotumiwa na wakazi pamoja na wafanyabiashara katika ukanda huo.
Kwa sasa, vyombo vya uokoaji na usalama vimefika eneo la tukio na vinaendelea na jitihada za kuhakikisha usalama wa wananchi pamoja na watumiaji wa barabara hiyo muhimu kwa shughuli za kiuchumi za wakazi wa maeneo hayo.
Mamlaka husika zinatarajiwa kutoa taarifa zaidi kuhusu hatua zinazochukuliwa kurejesha mawasiliano ya usafiri katika eneo hilo.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment